IRAQ-IS-USALAMA

Bett McGurk: Wanajihadi wa IS walioko Mosul kuuawa

Wapiganaji wa kundi la Islamic State (IS) hatimaye wamezingirwa katika eneo la Mosul magharibi, ngome kuu yao ya mwisho nchini Iraq, kwa sababu vikosi vya Iraq vimezoteka barabara zote zinazoingia na kutoka katika eneo hilo, amesema afisa wa Marekani.

AFP
Matangazo ya kibiashara

Bett McGurk afisa wa Marekani katika muungano wa kimataifa unaopambana dhidi ya IS amewambia waandishi wa habari Jumapili Machi 12 kwamba majeshi ya Iraq yameteka barabara zote zinazoingia Mosul Magharibi na hivyo kubaini kwamba wapiganaji wa Is wanaosalia katika eneo hilo watauawa.

"Wapiganaji wote wanaopatikana Mosul watauawao," amesema Bw McGurk. "Tumeamua si tu kupata ushindi Mosul, lakini pia kuhakikisha kwamba wapiganaji hao wasiwezi kututoroka."

Brett McGurk, ametoa onyo hilo baada ya wanajeshi wa Iraq kuteka njia pekee iliyokuwa ikitumiwa na wapiganaji hao kuondoka au kuingia mji huo.

Hii ina maana kwamba wapiganaji wa kundi hilo waliosalia mjini humo wamekwama.

Wapiganaji wa IS wamedhibiti mji huo wa pili kwa ukubwa nchini Iraq tangu 2014.

Lakini wanajeshi wa Iraq wamefanikiwa kuteka maeneo makubwa ya mji huo katika operesheni ya kijeshi iliyodumu kwa miezi kadha.

Kwa sasa, wanajeshi hao, wakisaidiwa na Marekani, wamefanikiwa kudhibiti maeneo yote ya mashariki mwa mji huo, kupitia vita hivyo vilivyoanza Machi 5.

Wamefanikiwa pia kuwafurusha wapiganaji hao kutoka sehemu muhimu upande wa magharibi wa mji huo, ikiwa ni pamoja na makao makuu ya baraza la mji pamoja na makumbusho makuu ya Mosul.

Hivi karibuni maafisa wa Marekani walikadiria kuwa wapiganaji 2,500 wa IS wanapatikana Magharibi mwa Mosul na katika mji wa Tal Afar, magharibi mwa Iraq.