ISRAEL-PALESTINA-USALAMA

Polisi ya Israel yamuawa muuaji kutoka Palestinav

Polisi wa Israel akifanya ukaguzi katika kata ya Jabel el Moukaber katika eneo la Jerusalem-Mashariki.
Polisi wa Israel akifanya ukaguzi katika kata ya Jabel el Moukaber katika eneo la Jerusalem-Mashariki. REUTERS/Ronen Zvulun

Jumatatu hii asubuhi Machi 13, raia mmoja wa Palestina amewajeruhi kwa kisu maafisa wawili wa kikosi cha ulinzi wa mipaka karibu na mji wa kale wa Jerusalem.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo polisi iliingilia kati na kumuua muuaji huyo, msemaji wa polisi ametangaza.

Muuaji, ambaye ni mkazi wa Jerusalem ya Mashariki, sehemu ya Palestina ya mji uliounganishwa na Israel, ameingilia katika eneo la mpaka ambapo aliwajeruhi maafisa wa wili wa kikosi cha ulinzi wa mipaka kabla ya kupigwa risasi.

Mmoja wa maafisa hao amejeruhiwa vibaya wakati ambapo wa pili alipata majeraha madogo, polisi imesem akatika taarifa yake.