SYRIA-MAREKANI-USALAMA

Msikiti washambuliwa Syria, Marekani yanyooshewa kidole

Msikiti wa Al-Bab mkoani Allepo, Machi 3, 2017.
Msikiti wa Al-Bab mkoani Allepo, Machi 3, 2017. REUTERS/Khalil Ashawi

Marekani yanyooshewa kidolea kuhusika na shambulio dhidi ya Msikiti nchini Syria. Lakini jeshi la Marekani linasema halikulenga Msikiti lcha ya kukiri kuendesha mashambulizi katika kijiji hicho kuliko sahmbuliwa Msikiti.

Matangazo ya kibiashara

Shirika la Haki za Binadamu nchini Syria la OSDH limebaini kwamba watu wasiopungua 42, wengi wao wakiwa ni raia wa kawaida wameuawa katika shambulio la angani lililoendeshwa dhidi ya Msikiti wa kijiji cha Al-Jineh, kilomita thelathini kutoka mji wa Aleppo.Zaidi ya watu mia moja walmejeruhiwa chanzo hicho kimesema.

Jeshi la Marekani limekiri kuwa liliendesha mashambulizi katika kijiji hicho, lakini linasema lilikua lililenga wapiganaji wa Al-Qaeda. Uchunguzi umeanzishwa ili kujua ukweli kuhusu shambulio hilo.

 "Hatukulenga msikiti, bali tulilenga jengo, ambapo kulifanyika mkutano wa hadhara wa Al-Qaeda, mita 15 kutoka Msikiti ambao bado uko imara," alisema Alhamisi jioni Kanali John J. Thomas, msemaji Centcom, uongozi wa vikosi vya Marekani katika Mashariki ya Kati.

"Tuchunguza madai kwamba mashambulizi hayo yamegharimu maisha ya watu wengi," alisema pia Kanali Thomas akihojiwa kuhusu idadi ya wahanga 42, wengi wao wakiwa raia wa kawaida.

Kwa mujibu wa Rami Abdel Rahman, mkurugenzi wa OSDH, zaidi ya watu mia moja pia walijeruhiwa katika mashambulizi hayo katika mji ulio chini ya udhibiti wa makundi ya waasi. Mapema Ijumaa asubuhi maafisa wa wa usalama wamekua wakijaribu kutafuta watu waliokwama chini ya vifusi vya Msikiti, kwa mujibu wa OSDH. Watu kadhaa bado hawajulikani walipo.