SOMALIA-YEMEN

Zaidi ya wasomali 40 wauawa nchini Yemen

Baadhi ya wakimbizi raia wa Somalia wameuawa mjini Hodeida nchini Yemen
Baadhi ya wakimbizi raia wa Somalia wameuawa mjini Hodeida nchini Yemen REUTERS/Abduljabbar Zeyad

Zaidi ya wakimbizi arobaini raia wa Somalia wameuawa katika shambulio lililolenga mashua waliyokuwa wakisafiria katika bahari ya shamu,wengi wao wanawake na watoto waliokuwa nchini Yemen.

Matangazo ya kibiashara

Bado haijajulikana kundi gani lililotekeleza shambulizi hilo lililojeruhi zaidi ya watu themanini.

Wakimbizi hao walishambuliwa kwa silaha za moto katika eneo linalodhibitiwa na waasi Hodeida lakini mashua yao ilifanikiwa kutia nanga katika bandari ya mji huo,kwa mujibu wa maafisa.

Shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi ambalo linafanya shughuli zake nchini Yemen limefahamisha kuwa maiti arobaini na mbili zimepatikana.

Maafisa wa bandari walisema Wasomali kadhaa walionusurika katika shambulio hilo wamepelekwa katika gereza moja mjini humo.

Majeruhi wote wamepelekwa hopsitali kupatiwa matibabu.