PALESTINA-MAREKANI-ISRAEL-USHIRIKANO

Mahmoud Abbas kukutana na Abdel Fattah al-Sissi kabla ya mkutano wake na Trump

Rais wa Palestina, Mahmoud AbbaS
Rais wa Palestina, Mahmoud AbbaS

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas anatarajiwa kukutana siku ya Jumatatu mjini Misri na mwenzake Abdel Fattah al-Sissi. Mkutano huu unakuja muda mfupi kabla ya mkutano wake na Rais wa Marekani Donald Trump.

Matangazo ya kibiashara

Mahmoud Abbas amepanga kutembelea Ikulu ya White House katikati mwa mwezi waAprili kwa ili kukutana uso kwa uso kwa mara yake ya kwanza na Donald Trump tangu bilionea huyu kuchukua hatamu ya uongozi nchini Marekani mwezi Januari mwa huu, afisa mmoja mwandamizi wa Palestina ameliambia shirika la habari la AFP, huku akitaomba jina lake sisitajwi.

Kabla ya hapo, na wakati ambapo mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa nci za Kiarabu utafanyika Machi 29 nchini Jordan, Rais wa Palestina atakutana na Bw Sissi, wakati ambapo mahusiano kati ya Wapalestina na Wamisri hivi karibuni yaliingiliwa na hali ya sintofahamu.

Kwa mujibu wa taarifa wa vyombo vya habari, Mfalme Abdullah II wa Jordan, moja ya nchi mbili tu za Kiarabu, pamoja na Misri, kutia saini mkataba wa amani na Israeli, pia akutana mwezi Aprili na Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye amesema anataka kushughulikia mgogoro wa zamani duniani iliu kutafutia suluhu ya kudumu.

Amman na Cairo, ambapo makao ni makuu ya Umoja nchi za za Kiarabu, ni washirika muhimu katika mchakato wa amani kati ya Israel na Palestina,, mchakato ambao umeshindikana kwa miaka kadhaa.