IRAQ-IS-MAPIGANO

Mapigano makali yarindima Mosul

Mosul, Machi 19, 2017. polisi ya Iraq yaendesha operesheni katika mji wa kale wa Mosul ambapo wamekimbilia wapiganaji wa IS.
Mosul, Machi 19, 2017. polisi ya Iraq yaendesha operesheni katika mji wa kale wa Mosul ambapo wamekimbilia wapiganaji wa IS. REUTERS/Thaier Al-Sudani

Mji wa kale wa Mosul unakabiliwa na mapigano makali, baada ya vikosi vya Iraq kuuzingira. wapiganaji wa kundi la Islamic State wamekimbilia katika sehemu hiyo ya jiji hilo kubwa, ambapo barabara ni finyu.

Matangazo ya kibiashara

Katika barabara hizo magari makubwa ya kijeshi, hasa vifaru, vimehindwa kupita. Askari wamelazimika kushika magari yao na kutembea kwa mguu. Hata hivyo kazi yao ni ngumu kwani wanakabiliwa na upinzani wa wapiganaji wa kundi la Islamic State, licha ya kusaidi na vikosi vya angani.

Helikopta za jeshi la Iraq jeshi zimekua zikishambulia ngome za wapiganaji wa kundi la Islamic State. Lengo la mashambulizi hao ya angani ni kuvunja upinzani au ulinzi wa mji wa kale wa Mosul.

"Pambano la mwisho la IS litachezwa katika mji huu wa kale, ambao ni mji wa usio kuwa na milima. Kama askari, ingelikua nataka kuweka mstari wa ulinzi ningelirudi nyuma kutoka mji huo, "amesema Kanali Fallah ambaye anaongoza operesheni hiyo ya kijeshi dhidi ya IS.

Hata hivyo mapigano ni makali, kwani hata wapiganaji wa kundi la Islamic State wanaonekana wamejihami vya kutosha. Moto unaendelea kuwaka katika mji wa Mosul na inaonekana mapigano hayo huenda yakaendelea usiku wa wa kuamkia Juamtatu hii