SYRIA-USALAMA

Eneo la Jobar lakumbwa na mapigano

Damascus, Machi 19, 2017. Moshi mkubwa katika eneo la Jobar, mashariki mwa mji mkuu wa Syria unaokumbwa na mapigano makali.
Damascus, Machi 19, 2017. Moshi mkubwa katika eneo la Jobar, mashariki mwa mji mkuu wa Syria unaokumbwa na mapigano makali. AMER ALMOHIBANY / AFP

Mapigano makali yalitokea siku ya Jumapili katika mji wa Damascus baada shambulizi la kushangaza la waasi na wapiganaji wa kijihadi kuelekea katikati mwa mji mkuu wa Syria. Serikali imeendesha mashambulizi kwa minajili ya kurejesha maeneo iliyopoteza.

Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hili ni moja ya mashambulizi mabaya kabisa kutokea Damascus tangu kuanza kwa vita, miaka sita iliyopita.

Mapigano hayo yalianza kwa mashambulizi mawili ya kujitoa mhanga kwa kutumia magari yaliyojaa vilipuzi dhidi yangome zai jeshi katika eneo la Jobar, karibu na eneo la Bani Abbas, mashariki mwa mji mkuu. Mapigano hayo yalitokea kilomita mbili na mji wa kale wa Damascus na eneo lenye watu wengi kutoka jamii ya Wakristo la Bab Touma. Washambuliaji wengine wa kujitoa mhanga waliotokea katika vichuguu viliyochimbwa katika eneo hilo, walishambulia askari wa Syria, wakifuatiwa na wapiganaji wengine kadhaa.

Wakati huo huo wapiganaji wa kijihadi walifaulu kuchukua udhibiti wa majengo kadhaa, na walirusha makombora na roketi katika mji mkuu.

Hata hivyo jeshi la Syria lilikabiliana na mashambulizi hayo. Jeshi la nci kavu na kikosi cha angani vilisaidia kwa kuendesha operesheni kwa pamoja kwa muda wa masaa kadhaa kabla ya kikosi maalumu kutumwa katika maneo hayo ya vita.

Milio ya risasi na milipuko ya mabomu vilisikika mjini kote Damascus. Baada ya mapigano makali, jeshi lilifaulu kudhibiti hali ya mambo katika uwanja wa vita, na kisha kuzirejesha ngome zao zilikua zimeshikiliwa na wanajihadi.