Shambulio dhidi ya shule laua watu wasiopungua 33 karibu na Raqqa
Imechapishwa:
Watu wasiopungua 33 wameuawa karibu na mji wa Raqqa, nchini Syria, katika mashambulizi ya angani dhidi ya shule wanakopewa hifadhi wakimbizi wa ndani nchini humo, shirika la Haki za Binadamu (OSDH) limearifu Jumatato wiki hii.
OSDH imeongeza kuwa inaonekana kwa shule hilo lilishambuliwa na muungano wa kimataifa dhidi ya IS unaoongozwa na Marekani.
Pentagon imesema hawana taarifa yoyote inayosema kuwa mashambulizi yaliyondeshwa na muungano wa kimataifa yaliwaathiri raia, lakini imesema uchunguzi utafanyika.
"Hatuna taarifa ambayo inasem akuwa mashambulizi ya angani yaliwaathiri raia karibu na mji wa Raqqa kama linavyosema shirika la Haki za Binadamu nchini Syria (OSDH)," imesema Pentagon katika taarifa hiyo.
Mashambulizi hayo yalitokea siku ya Jumatatu usiku katika kijiji cha Al Mansoura, magharibi mwa mji wa Raqqa, ngome ya kundi la Islamic State (IS) nchini Syria, alisema mkurugenzi wa OSDH, Rami Abdulrahman.