Waasi nchini Syria wauteka uwanja wa kijeshi mjini Raqa
Imechapishwa:
Waasi wanaoungwa mkono na Marekani nchini Syria wanasema wamefanikiwa kuuteka uwanja wa ndege wa kijeshi mjini Raqa.
Mji huo kwa muda mrefu umekuwa ukidhibitiwa na wapiganaji wa Islamic State kwa muda mrefu wakati huu wakiendelea kukabiliwa.
Msemaji wa waasi hao Talal Sello, amethibitisha kuuchukua uwanja huo wa Tabqa ambao umekuwa mikononi mwa Islamic State tangu mwaka 2014.
Mafanikio ya wapiganaji hawa wa waasi yanakuja wiki moja baada ya Ufaransa kutangaza kuwa muungano wa kijeshi wa nchi za Magharibi hivi karibuni wataanzisha operesheni ya kuwaondoa kabisa Islamic State katika ngome yao ya Raqa.
Mzozo wa Syria ulioanza mwaka 2011, umeshabisha zaidi ya watu 300,000 kupoteza maisha.
Mazungumzo ya amani yanayoendelea jijini Geneva nchini Uswizi kati ya serikali ya Damascus na wapinzani bado hajawafanikiwa.