SYRIA-MAREKANI

Trump alaani shambulizi la silaha za kemikali nchini Syria

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump Reuters

Rais wa Marekani Donald Trump amelaani shambulizi la silaha za kemikali lililosababisha zaidi ya watu 70 nchini Syria wakiwemo watoto.

Matangazo ya kibiashara

Trump amesema kuwa shambulizi hilo limevuka mpaka na halikubaliki kamwe.

“Unapoua watoto wadogo, wasio na makosa, watoto wadogo, hakika ni kuvuka mipaka mingi,” alisema Trump.

Hata hivyo, hakuitaja Urusi ambaye ni mshirika wa karibu sana Syria.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Nikki Haley hata hivyo, ameishutumu Urusi kwa kuilindia kifua serikali ya Syria baada ya kutekeleza shambulizi hilo.

“Mara kwa mara, Urusi unatumia uongo kuilinda serikali ya Damascus inapotekeleza mashambulizi kama haya,” ameongeza Nikki Haley.

Mataifa ya Magharibi yameishutumu serikali ya Syria, kutekeleza mashambulizi hayo lakini rais Bashar al-Assad amekanusha madai hayo.

Urusi nayo inasema mashambulizi hayo yalitekelezwa na waasi wanaoipinga serikali ya Assad.