PALESTINA-HAMAS-USALAMA

Hamas yakubali kuundwa kwa taifa la Palestina

Kiongozi wa kamati kuu ya kisiasa ya kundi la Hamas, Khaled Mechaal katika mkutano na waandishi wa habari mjini Doha, Mei 1 2017.
Kiongozi wa kamati kuu ya kisiasa ya kundi la Hamas, Khaled Mechaal katika mkutano na waandishi wa habari mjini Doha, Mei 1 2017. KARIM JAAFAR / AFP

Kundi la Hamas, siku ya Jumatatu, limetangaza kuwa linakubali kuundwa kwa taifa la mpito la Palestina lenye mipaka iliyopatikana baada ya vita vya siku sita katika mwaka 1967.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo la kundi la kiislamu la Hamas linabadili kwa mara ya kwanza katika historia yake mpango wake wa kisiasa juu ya suala hili.

Taifa hilo ni lile lililowekwa na chama cha Fatah, kinachoongozwa na rais wa Palestina Mahmoud Abbas na mpinzani wa kundi la Hamas, ambalo linasimamia Ukanda wa Gaza kwa miaka kumi.

"Hamas linapigana kwa ajili ya ukombozi wa taifa lote la Palestina lakini inaunga mkono taifa lenye mipaka iliyopatikana katika mwaka 1967, bila hata hivyo kuitambua Israel au kuipa haki yoyote," alisema kiongozi wa kisiasa wa Hamas, Khaled Mechaal, akiwa mjini Doha.

Wakati wa mgogoro ulioendeshwa miaka hamsini iliyopita dhidi ya nchi za Kiarabu, Israel ilichukua udhibiti wa Gaza, Ukingo wa Magharibi na Mashariki mwa Jerusalem. Seikali ya Kiyahudi iliondoka Gaza mwaka 2005.

Hamas inachukuliwa kama shirika la kigaidi na Marekani, Umoja wa Ulaya na Israel. Tangazo hili linakuja siku mbili kabla ya mkutano wa kwanza katika Ikulu ya White House kati ya Rais Mahmoud Abbas na Donald Trump.