PALESTINA-MAREKANI-USHIRIKIANO

Mahmoud Abbas kukutana na Donald Trump Washington

Rais wa Mamlaka yaPalestina Rais Mahmoud Abbas anatazamiwa kuwasili Washington.
Rais wa Mamlaka yaPalestina Rais Mahmoud Abbas anatazamiwa kuwasili Washington. REUTERS/Issam Rimawi/Pool/File Photo

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas anatazamiwa kupokelewa Jumatano hii Mei 3 katika Ikulu ya White House, mjini Washington. Huu utakuwa mkutano wa kwanza wa kiongozi wa Palestina na Rais wa Marekani. Donald Trump atakuwa na mazungumza na kiongozi wa Palestina, ambaye mamlaka yake yanaonekana kuwa hatarini.

Matangazo ya kibiashara

Kabla ya uchaguzi, Donald Trump alionyesha msimamo wake ambapo aliunga mkono Israel kuendelea na ujenzi wa makazi ya walowezi wa kiyahudi katika maeneo ya Palestina. Bw Trump aliahidi kuhamisha ofisi za ubalozi wa Marekani kutoka mji wa Te-Aviv kwenda Jerusalem, akishtumu utawala wa Barack Obama kupitishi azimio lililolaani Israel kwa kuendelea kujenda makaazi ya walowezi katika maeneo ya Palestina.

hatimaye mambo yamebadilika. Hakuna suala la kuhamisha ofisi za ubalozi wa Marekani. Na wakati wa ziara ya Benjamin Netanyahu mjini Washington, rais Trump alimuelezea kinaga ubaga kwamba ujenzi wa makazi mapya hayaendani na njia ya amani.

Leo, vyombo vya habari vya Marekani vinaamini kuwa Donald Trump atamuomba Mahmoud Abbas kuacha kulipa pensheni kwa familia za wapiganaji waliuawa na jeshi la Israel. Sera ya Trump katika Mashariki ya Kati haiko wazi wazi, pamoja na kwamba katika mahojiano ya hivi karibuni, alisema alitaka yafikiwe makubaliano ya amani ambayo anaona ni muhimu. Donald Trump tayari amekutana na mwenzake wa Misri na mfalme wa Jordan. alipeleka suala hilo kwa mkwewe na mshauri wake wa karibu, Jared Kushner.