AFGHANISTAN-NATO-USALAMA

Shambulio baya latokea dhidi msafara wa NATO mjini Kabul

Shambulio lilitokea karibu na ubalozi wa Marekani mjini Kabul, Mei 3, 2017.
Shambulio lilitokea karibu na ubalozi wa Marekani mjini Kabul, Mei 3, 2017. REUTERS/Mohammad Ismail

Msafara wa majeshi ya kigeni waliokua wakipiga doria karibu na ubalozi wa Marekani katikati mwa mji wa Kabul umekumbwa na shambulio mapema Jumatatu hii Mei 3 asubuhi. askari 8 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya ishirini wamejeruhiwa, wengine wao wakiwa ni raia wa kawaida, wamesema maafisa wa Afghanistan.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio ambalo lilikua limelenga "msafara wa majeshi ya kigeni katika eneo hilo," limegharimu maisha ya watu 8 na 25 kujeruhiwa, "wengine wao wakiwa ni raia wa kawaida," amesema msemaji wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghanistan, Najib Denmark, akinukuliwa nana shirika la habari la AFP.

Kwa mujibu wa chanzo cha usalama cha Afghanistan, bomu lililotegwa katika gari ndogo limelenga msafara wa majeshi ya Marekani yaliyokua yakipiga doria karibu na ubalozi wa Marekani na makao makuu ya Resolution Support, kikosi cha muungano wa nchi za kujihami za magharibi (NATO) nchini Afghanistan. Chanzo hiki kimearifu kwamba watu 8 wameuawa na wengine 22 walijeruhiwa pamoja na askari watatu wa Marekaniambao walipata majeruhi madogo lakini wameondolewa haraka kutoka eneo hilo.

Mpaka sasa hakuna kundi amblo limedai kuendesha shambulio hilo. Shambulio hiulo linatokea siku chache baada ya tangazo la kundi la Taliban la kuanzisha mashambulizi makali dhidi ya vikosi vya kigeni.