PALESTINA-MAREKANI-USHIRIKIANO

Trump ampokea Abbas mjini Washington

Mahmoud Abbas (kushoto) nat Donald Trump, Mei 3, 2017 White House, Washington.
Mahmoud Abbas (kushoto) nat Donald Trump, Mei 3, 2017 White House, Washington. REUTERS/Carlos Barria

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amepokelewa Jumatano katika Ikulu ya White House na rais wa Marekani Donald Trump, ambaye alisema ana imani kwambai "kitu cha ajabu" kinatazamiwa kutokea kati ya Palestina na Israel.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani ameahidi kufanya kazi pamoja na Israel na Palestina ili kufikia makubaliano ya amani na ametoa wito kwa viongozi wa Palestina "kuzungumza kwa kauli moja dhidi uchochezi" wa machafuko.

Wakati huo huo Mahmoud Abbas amekumbusha ahadi yake ya ufumbuzi kwa mataifa hayo mawili kulingana na mipaka ya 1967, kabla ya Ukingo wa Magharibi, Gaza na Jerusalem Mashariki kushikiliwa na Israeli.

Donald Trump alimpokea Februari 15 Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu. Wakati huo aliahidi kusaidia lengo la mkataba wa amani kati ya Israel na Palestina bila hata hivyo kutangaza kuwa anaunga mkono ufumbuzi kati ya Israel Na Palestina, jambo ambalo haijafanya mbele ya Mahmoud Abbas.

"Tutaweza kuendeleza mambo," aliahidi Donald Trump kwa rais wa Palestina akionyesha Marekani kama "mpatanishi, msimamizi au mwamuzi" kati ya kambi hizo mbili.

"Mara zote nilisikia kwamba mkataba mgumu sana wa kufikia ni labda ule kati ya Israel na Palestina," aliongeza rais wa Marekani. "Hebu tuwalaumu."

Mvutano kati ya mataifa haya mawili umeendelea kukua na watu wengi wamepoteza maisha katika machafuko yanayoendelea kati nchi hizi.