SYRIA-MAREKANI-HAKI

Syria yakanusha shutuma za Marekani kuhusu kuchomwa kwa wafungwa

Picha ya Satellite ya gereza la Saydnaya, ilio katika ripoti iliyochapishwa mwezi Februari na Amnesty International.
Picha ya Satellite ya gereza la Saydnaya, ilio katika ripoti iliyochapishwa mwezi Februari na Amnesty International. © Amnesty International/Forensic Architecture

Ufaransa imeomba uchunguzi wa kimataifa baada ya madai mapya yaliyotolwa na Marekani dhidi ya serikali ya Syria. Serikali ya Marekani imeshtumu Syria kuwa iliwachoma baadhi ya maelfu ya wafungwa katika jela, wafungwa ambao waliuawa katika miaka ya hivi karibuni.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Syria imefutilia mbali shutma hizo, ikibaini kwamba ni "uzushi usiokuwa na msingi" wa utawala wa Marekani.

Hizi ni tuhuma nzito ambazo zilitolewa na Marekani dhidi ya serikali ya Syria. Kwa mujibu wa serikali ya Marekani, Syria ilichoma maelfu ya miili ya wapinzani katika jengo lililo karibu na gereza la Saydnaya, kaskazini mwa mji mkuu wa Syria.

Washington inadai kuwa ushahidi kupitia picha za setilaiti na ripoti iliyochapishwa mwezi Februari na shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International. Katika ripoti hii, shirika hilo linaishtumu serikali ya Syria linatamia jela hilo kama sehemu ya machinjo ya binadamu.

Siku ya Jumanne, Syria ilifutilia mbali madai yaliyotolewa na utawala wa Marekani. "Madai haya hayana msingi kabisa" na yalitengenezwa na watu wasijua hali halisi," Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Syria imesema.

Nchini Ufaransa, seikali imesem amadai ya Marekani yana ukweli fulani , huku ikiomba kufanyika kwa haraka uchunguzi wa kimataifa kuhusu masaibu yaliyotokea katika gereza la Saydnaya.