IRAN-MAREKANI

Baada ya ushindi,Marekani yamtaka Rouhan kukomesha Ugaidi Iran

Kwa mara ya pili Hassan Rouhan amechaguliwa kuongoza taifa la Iran
Kwa mara ya pili Hassan Rouhan amechaguliwa kuongoza taifa la Iran President.ir/Handout via REUTERS/File Photo

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Rex Tillerson amemtaka raisi wa Iran Hassan Rouhani kuharibu mtandao wa ugaidi unaofanywa na Tehran na kukomesha majaribio yake ya makombora,ikiwa ni kauli ya kwanza kutolewa na Marekani baada ya kushinda kiti cha uraisi.

Matangazo ya kibiashara

Akiwa Riyadh Tillerson amesema anatumaini kuwa raisi Rouhan ataitumia fursa nyingine ya kuongoza Iran kukomesha mtandao wa kigaidi unaoyumbisha usalama katika ukanda huo.

Raisi wa Iran Hassan Rouhani ameshinda kwa mara nyingine uchaguzi wa raisi nchini humo kwa asilimia 57 ya kura wizara ya mambo ya ndani imefahamisha.

Jumla ya asilimia 99.7 ya kura zilizohesabiwa Rouhani alijipatia kura milioni 23.5 zaidi ya mshindani wake wa karibu Ebrahim Raisi ambaye alipata kura milioni 15.8 kwa mujibu wa matokeo ya mwisho.

Aidha Viongozi mbalimbali wa kimataifa wamempongeza Rouhan kwa ushindi huo akiwemo raisi wa Urusi Vladir Putin ambaye ameitaka ushirikiano kuimarishwa zaidi kati ya Tehran na Moscow.