MAREKANI-ISRAEL-PALESTINA-TRUMP

Donald Trump kuzuru Jerusalem na Palestina Jumatatu hii

Donald Trump nchini Saudi Arabia Mei 21, kabla ya safari yake kwa ziara ya saa 24 nchini Israël.
Donald Trump nchini Saudi Arabia Mei 21, kabla ya safari yake kwa ziara ya saa 24 nchini Israël. REUTERS/Jonathan Ernst

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajiwa kufanya ziara nchini Jerusalem Jumatatu hii, Mei 22. Rais wa Donald Trump anaanza ziara yake ya kwanza ya siku mbili nchini Israeli na Palestina.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani atazuru maeneo matakatifu ya Ukristo na Uyahudi. Pia atakutana na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas.

Donald Trump atahutubia wananchi wa mataifa hayo mawili ambapo atazungumzia kuhusu mgogoro kati ya Israel na Palestina. Bado watu wengi wanajiuliza iwapo atasikilizwa, kwa sababu Wapalestina wengi hawana imani naye, hata baadhi ya Waisrael bado wana mashaka naye.

56% ya raia wa Kiyahudi nchini Israel hawamuoni Donald Trump kama mtu aliye karibu na Israel.

Kabla ya kuchukua hatamu ya uongozi wa Marekani, Donald trump aliungwa mkono na idadi kubwa ya Wayahudi, na kwa wakati huu idadi inayomuunga mkono rais huyo wa Marekani imeshuka kwa sababu mbalimbali.

Baadhi ya Wayahudi wanamuona kama mfanyabiashara tu ambaye hana muono na hajabobea kisiasa.

Ahadi yake ya kuhamishia ubalozi wa Marekani katika mji wa Jerusalem kutoka Tel Aviv haupewi tena kipaumbele, na sehemu ya vyama vya mrengo wa kulia pia inalaani kusita kwake kwa kuunga mkono Israe kuendelea kushikilia baadhi ya maeneo ya Palestina.

Kuna Wayahudi ambao wanamuunga mkono rais huyo wa Marekani hasa kwa kile wanachosema kuwa kusitisha ujenzi wa nyumba za walowezi wa Kiyahudi katika maeneo ya Palestina ni jambo muhimu kwa usalama wa mataifa hayo mawali. Hoja hii ilitolewa na rais wa Marekani Donald Trump.

Hata hivyo Donald Trump ameendelea kukosolea nchini Israel kutokana na
tabia yake ya ubaguzi wa kijinsia na ubaguzi wa rangi.