UFARANSA-URUSI-USHIRIKIANO

Macron na Putin wazungumzia kuhusu Syria na Ukraine

Rais wa Urusi Vladimir Putin (kushoto) na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia) katika mji wa Versailles, Mei 29.
Rais wa Urusi Vladimir Putin (kushoto) na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia) katika mji wa Versailles, Mei 29. REUTERS/Philippe Wojazer

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macro na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin walikutana jana katika jitihada za kuimarisha uhusiano kati ya mataifa hayo mawili.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wamesema mazungumzo yao kuhusu maswala mbalimbali ikiwemo machafauko nchini Syria na Ukraine yamekuwa ya wazi.

Kuhusu Syria, rais Macron amesema wanatofatiana kuhusu nam na ya kutatua mzozo wa Syria, lakini serikali ya Ufaransa inaiunga mkono vita dhidi ya ugaidi.

Huu ulikuwa mkutano wa kwanza kati ya rais Macron na rais Putin.

Mataifa hayo yanaadhimisha pia miaka 300 ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.