QATAR-UGAIDI-USALAMA

Mgogoro katika Ghuba: Qatar yashinikizwa

Doha, Qatar, Juni 5, 2017.
Doha, Qatar, Juni 5, 2017. Reuters

Mara tu baada ya kutangazwa kuvunjika kwa uhusiano wa kidiplomasia, uamuzi ambao ulichukuliwa na Saudia Arabia na washirika wake dhidi ya Qatar, Iran imewatolea wito majirani zake wa Ghuba kufanya "mazungumzo ya wazi" kwa kutatua migogoro yao.

Matangazo ya kibiashara

Saudi Arabia, Misri, Falme za Kiarabu na Bahrain waliamua siku ya Jumatano Juni 5 kuvunja uhusiano wao wa kidiplomasia na Qatar na hasa kuamua kufunga anga yao na mipaka yao ya ardhini na majini na nchi hii ndogo, lakini tajiri kwa mafuta na hasa gesi. Kuvunjika kwa uhusiano na Doha kumetokana na "kuunga mkono ugaidi", ikiwa ni pamoja na al-Qaeda, kundi la Islamic State (IS) na Muslim Brotherhood, kundil ililotangazwa la "kigaidi" na Misri na nchi za Ghuba. Kwa mujibu wa Riyadh, Doha pia inasaidia "shughuli za kigaidi za makundi yanayoungwa mkono na Iran katika jimbo la Qatif (mashariki)", ambapo wanaishi watu wachache kutoka jamii ya Mashia katika ardhi ya Saudi Arabia, pamoja na Bahrain,inayokumbwa kwa miaka kadhaa na machafuko yanayoendeshwa na idadi kubwa ya Mashia nchini humo.

Wakati huo huo Tehran imetoa pendekezo baada ya Saudi Arabia na washirika wake kutangaza kuvunjika kwa uhusiano wa kidiplomasia na Qatar. "Utatuzi wa migogoro katika nchi za kanda Ghuba, ikiwa ni pamoja na matatizo ya sasa kati ya majirani watatu Qatar na nchi hiyo unawezekana tu kwa njia ya kisiasa na amani na mazungumzo ya kweli kati ya pande zinazokinzana", alisema siku ya Jumatatu Bahram Ghasemi, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, katika taarifa yake.

Qatar na Iran wana mahusiano kwa miongo kadhaa, hali ambayo haifurahishi Saudi Arabia na rais wa Marekani Donald Trump. Nchi hizi mbili zina mahusiano tangu kuundwa kwa taifa la Qatar mwaka 1971. Doha ina mahusiano na Tehran kwa sababu kuu mbili: ghala la pamoja la gesi na nia ya kukabialiana na Saudi Arabia.