QATAR-UGAIDI-USALAMA

Nchi 4 za kiarabu zavunja uhusiano wao na Qatar

Nchi kadhaa za muungano wa ushirikiano wa Ghuba zavunja uhusiano wa kidiplomasia.
Nchi kadhaa za muungano wa ushirikiano wa Ghuba zavunja uhusiano wa kidiplomasia. AFP PHOTO/YASSER AL-ZAYYAT

Nchi nne za Kiarabu ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia, Misri, Bahrain na Umoja wa Nchi za Kiarabu wamevunja uhusiano wao wa kidiplomasia na nchi ya Qatar wakiisishtumu kuhusika au kuchangia kwa njia moja ama nyinge kwa kuvuruga ukanda huo.

Matangazo ya kibiashara

Nchi hizi nne zimeishtumu Qatar kuunga mkono na kusaidia ugaidi. Qatar imelaumiwa kusaidia na kuunga mkono kundi la Muslim Brotherhood, lililopigwa marifuku nchini Misri.

Shirila la taifa la habari nchini Bahrain limesema kuwa nchi hiyo inavunja uhusiano wake na Qatar kwa hatarisha usalama wake.

Misri imefunga anga zake na bandari ya Qatar, kwa mujibu wa wizara ya mashauri ya nchi kigeni.

Saudi Arabia imefunga mipaka yake na kusitisha usafiri wa ardhini, baharini na angani, kwa mujibu wa chanzo cha serikali.

Kwa mujibu wa chanzo hiki, maafisa wamesema kuwa hatua hiyo ni ya kulinda usalama wa nchi kutokana na hatari za ugaidi na itikadi kali.

Bahrain imewapa wanadiplomasia wa Qatar saa 48 kuondoka nchini humo. Baharain inailaumu Qatar kwamba imekua ikiendelea harakati zake za kufadhili ugaidi na itikadi kali.