MAREKANI-QATAR-UGAIDI

Donald Trump akaribisha hatua ya Saudi Arabia dhidi ya Qatar

rais wa Marekani Donald Trump aisifu Saudi Arabia kwa hatua yake dhidi ya Qatar.
rais wa Marekani Donald Trump aisifu Saudi Arabia kwa hatua yake dhidi ya Qatar. REUTERS/Jonathan Ernst

Rais wa Marekani Donald Trump ameyataka mataifa ya Ghuba kuungana katika vita dhidi ya ugaidi na itikadi kali, baada ya kuusifu msimamo wa Saudi Arabia wa kuitenga nchi jirani baada ya Qatar kushtumiwa kusaidia kifedha makundi yenye msimamo mkali.

Matangazo ya kibiashara

Trump ameoa kauli hii baada ya kumpigia simu Mfalme Salman wa Saudi Arabia na kumhakikishia kuwa anaunga mkono hatua ambayo ilichukuliwa na mataifa kadhaa ya kiarabu kusitisha ushirikiano wa kidiplomasia na Qatar kwa mada kuwa inaunga mkono makundi ya kigaidi.

Trump ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba hatua hiyo inaweza kuwa ndio mwanzo wa kutokomeza tishio la ugaidi.Katika mkutano na waandishi wa habari, msemaji wa ikulu ya Marekani, Sean Spicer, amesema mgogoro huo umekuwa ukifukuta kwa muda mrefu.

Qatar imekanusha madai hayo, huku Kuwait na Uturuki zikitaka kufanyika kwa mazungumzo ya haraka kurejesha hali ya ushirikiano.

Wakati huo huo, nchi kadhaa ikiwemo Uturuki, zimeonyesha wasiwasi wake kutokana na kuzorota kwa uhusiano katika eneo hilo la Ghuba.

Rais wa Uturuki amejitolea kupatanisha mgogoro huo huku akisema kutengwa na vikwazo havitatatua mgogoro huo.

Hali hii imeanza kushuhudiwa nchini Qatar ambako maduka mengi yameanza kusalia bila vyakula kwa sababu wamekuwa wakitegemea kutoka Saudi Arabia.