SAUDI ARABIA

Mfalme Salman amteua mwanaye wa kiume kumrithi

Mwanafalme wa Saudi Arabia  Mohammed bin Salman
Mwanafalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman REUTERS/Charles Platiau/File Photo

Mfalme wa Saudi Arabia amemteua mtoto wake wa kiume Mohammed bin Salman kama Mwanamfalme anayechukua  nafasi ya mpwa wake Mohammed bin Nayef.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa Mfalme Salman unamaanisha kuwa mwanaye Mohammed bin Salman mwenye umri wa miaka 31, atakuwa Naibu Waziri na wakati uo huo Waziri wa Ulinzi.

Baada ya kuondolewa katika nafasi hiyo, Mohammed bin Nayef mwenye umri wa miaka 57 ameapa kumtii Mwanamfalme mpya.

Saudi Arabia imekuwa ikiongozwa na Wafalme kuanzia miaka ya 70 na 80.

Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa uamuzi wa Mfalme Salman ni ishara kuwa nchi hiyo inaelekea kupata uongozi mpya.