IRAQ-IS-USALAMA

Kundi la IS lalipua msikiti wa kihistoria wa Al-Nuri mjini Mosul

Serikali ya Iraq imelishtumu kundi la IS kulipua msikiti wa kihistoria wa Al-Nuri mjini Mosul.
Serikali ya Iraq imelishtumu kundi la IS kulipua msikiti wa kihistoria wa Al-Nuri mjini Mosul. REUTERS/Stringer

Kundi la Islamic State limelipua msikiti wa kihistoria wa Al-Nuri mjini Mosul nchini Iraq, walikotangazia kuanza harakati zao. Hata hivyo wanamgambo wa IS wanadai kwamba ndege za jeshi la Marekani ndiyo zilizo zilizolipua msikiti huo.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Iraq limethibitisha kuharibiwa kwa msikiti huo wakati huu likiendeleza juhudi za kuwoandoa wapiganaji hao katika mji huo.

Miaka mitatu iliyopita, kiongozi wa kundi hilo Abu Bakr al-Baghdadi akiwa ndani ya msikiti huo alitangaza kudhibiti maeneo kadhaa nchini Syria na Iraq.

Serikali ya Iarq imesema kilichoteekelezwa na Islamic State ni sihara tosha kuwa limeshindwa katika makabiliano yanayoendelea kudhibiti mji wa Mosul.

Hata hivyo shirika la habari linalomilikiwa na kundi hilo la Amaq limedai kuwa, wanajeshi wa Marekani ndio walioshambulia msikiti huo, madai ambayo Marekani imekanusha.