IRAQ-ISIS

Makabiliano makali yazuka Magharibi mwa mji wa Mosul

Makabiliano katika mji wa Mosul nchini Iraq
Makabiliano katika mji wa Mosul nchini Iraq REUTERS/Alaa Al-Marjani

Wanajeshi wa Iraq wameendeleaza msako na mashabumbulizi makali dhidi ya wapiganaji wa Islamic State Magharibi mwa mjini Mosul.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa watu kadhaa wameuawa na wengine kujeruhiwa katika makabiliano hayo siku ya Jumatatu.

Wakaazi wa maeneo ya mji huo ya Tanak na Yarmuk, wanaishi kwa hofu baada ya kundi la Islamic State na kuanza kusabibisha wakaazi wa eneo hilo la mji kukimbilia usalama wao.

Jeshi la Iraq linasema kuwa kati ya wapiganaji 15-20 waliuawa katika mashambulizi hayo.

Operesheni dhidi ya Islamic State ilianza mwezi Oktoba mwaka uliopita katika ngome yake ya Mosul na hadi sasa zaidi ya watu 800,000 wameyakimbia makwao.