SYRIA

Ndege ya kivita yauwa watu 30 nchini Syria

Ndege ya kivita ya Urusi ikiwa nchini Syria
Ndege ya kivita ya Urusi ikiwa nchini Syria intelligencebriefs.com

Mashirika ya kutetea haki za binadmau nchini Syria yanasema, shambulizi la angaa limesababisha vifo vya watu 30 Mashariki mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa shambulizi hilo limetokea katika eneo la al-Dablan.

Haijafahamika  wamiliki wa ndege iliyotekeleza shambulizi hilo kwa mujibu wa ripoti ya muungano wa mashirika hayo ya kutetea haki za binadamu.

Muungano wa mataifa yanayoshirikiana na Marekani pamoja na zile za Urusi, zimekuwa zikishambulia kundi la Islamic State nchini Syria.

Siku ya Jumatatu, shambulizi kama hili lilitekelezwa katika eneo la al-Mayadeen na kusababisha vifo vya watu  57.

Hakuna aliyejitokeza na kudai kutekeleza shambulizi hili la siku ya Jumatano.