Saudi Arabia na washirika wake kuendelea kuitenga Qatar
Imechapishwa:
Mawaziri wa kigeni wa nchi nne ambazo zimeitenga Qatar, ikiwa ni pamoja na Saudi Arabia, Misri, Falme za Kiarabu na Bahrain walikutana Cairo siku ya Jumatano Julai 5 kujadili athari za hatua dhidi ya nchi hiyo.
Katika taarifa ya pamoja, walisema watadumisha vipimo vya "kuitenga Qatar kama itaendelea na uungwaji wake mkonona msimamo mkali na ugaidi. mkutano mpya Umepangwa kufanyika Manama nchini Bahrain.
Taarifa ya nchi hizi nne inasema hakuna hoja ya kuondoa vikwazo dhidi ya Qatar. Nchi hizi nne zinaonyesha kwamba hakuna suala la kuondoa vikwazo dhidi ya Qatar kama nchi imekubali kushiriki katika mapambano dhidi ya siasa kali na ugaidi.
Waziri wa Mambo ya nje wa Qatar anataka kufanyika kwa mazungumzo na mataifa mengine ya kiarabu ili kumaliza mvutano unaondelea.
Waziri huyo Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al-Thani amesema mazungumzo pekee ndio yanayoweza kutatua mvutano huu wa madai kuwa inaunga mkono ugaidi na kusema ni hatua ya kujaribu kuingilia uhuru wa nchi yake.
Wito huu umekuja Mawaziri wanne wa mataifa ya kiarabu wakikutana jijini Cairo nchini Misri, kuamua kuichukulia Qatar hatua zaidi.
Mataifa hayo yalikuwa yametia saa 48 kwa Qatar kufunga kitruo chake cha Aljazeera katika mataufa hayo kwa madai kuwa kinatumiwa kufadhili ugaidi.