UAE-QATAR-USHIRIKIANO

Waziri wa Falme za Kiarabu akanusha madai ya Washington Post

Doha, mji mkuu wa Qatar.
Doha, mji mkuu wa Qatar. STR / AFP

Waziri wa Mambo ya nje wa Falme za Kiarabu Anwar Gargash, amekanusha madai yaliyochapishwa na Gazeti la Marekani la Washington Post kuwa, ilidukua tovuti za serikali za Qatar.

Matangazo ya kibiashara

Garwash amesema madai hayo ni ya uongo na kuongeza kuwa alikuwa na uhakika kuwa taarifa hiyo ya Washingtin Post itatoweka hivi karibuni.

Katika hatua nyingine, Waziri huyo amesema kuwa Qatar huenda ikaondolewa kabisa katika Baraza la nchi za Ghuba ikiwa itaendelea kuhatarisha usalama wa ukanda huo na kuitaka kubadilisha tabia yake.

Hivi karibuni nchi za Kiarabu zaidi ya nne za Ghuba zilichukua hatua ya kusitisha uhusiano wa kidilpomasia na nchi ya Qatar zikiishtumu kwamba imekua ikichochea ugaidi katika ukanda huo, hatua ambayo ilikaribishwa na Marekani.