QATAR-DIPLOMASIA-USALAMA

Qatar yatakiwa kutekeleza mambo sita muhimu ili kuondolewa vikwazo

Mawazir wa Mambo ya nje kutoka nchi za kiarabu waliokutana hivi karibuni jijini Cairobi nchini Misri
Mawazir wa Mambo ya nje kutoka nchi za kiarabu waliokutana hivi karibuni jijini Cairobi nchini Misri REUTERS/Khaled Elfiqi

Saudi Arabia, Falme za Kiarabu, Misri na Bahrain zinaitaka Qatar kuunga mkono mambo sita waliyokubaliana kwa lengo la kupambana na ugaidi katika eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kuhakikisha kuwa makundi ya kigaidi hayapati fedha za kuendeleza harakati zao.

Wito huu umekuja wakati huu Qatar ambayo imetengwa ikiendelea kukanusha madai kuwa inaunga mkono makundi ya kigaidi.

Mataifa hayo pia yamekuwa yakiitaka Qatar kukifunga kituo cha Al Jazeera ambacho kinadaiwa kupeperusha na kufanikisha ajenda na makundi ya kigaidi.

Marekani na Mataifa mengine ya Magharibi yamekuwa yakitoa wito kwa Mataifa hiyo ya kiarabu kutafuta mwafaka na Qatar kupitia njia ya mazungumzo.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson alizuru mataifa ya Mashariki ya Kati kujaribu kutafuta mwafaka lakini akarudi nyumbani mikono mitupu.