SYRIA-USALAMA

Mji wa Idleb waanguka mikononi mwa kundi la kijihadi la Tahrir al-Sham

Moshi mkubwa wasuhudiwa katika kambi ya jeshi inayodhibitiwa na waasi wa kundi la Ahrar al-Sham, katika eneo la Idleb.
Moshi mkubwa wasuhudiwa katika kambi ya jeshi inayodhibitiwa na waasi wa kundi la Ahrar al-Sham, katika eneo la Idleb. REUTERS/Khalil Ashawi

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa shirika la Haki za Binadamu nchini Syria la OSDH, mji wa Idleb kaskazini magharibi mwa Syria, tangu Jumapili Julai 23 uko chini ya udhibiti wa kundi la kijihadi la Tahrir al-Sham, baada ya kuondoka kwa kundi hasimu la waasi.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano kati ya wapiganaji wa kijihadi wa kundi la Tahrir al-Sham na mahasimu wao wa kundi la Ahrar al-Cham yalidumu kwa siku mbili tu. Tawi la zamani la al-Qaeda nchini Syria tangu siku ya Jumapili limechukua udhibiti wa mji mkuu wa jimbo la Idleb baada ya kuondoka kwa wapiganaji wa Ahrar al-Sham kuelekea katika mji wa Sahl al-Ghab katika mkoa wa kati wa Hama.

Kabla kusitishwa kwa mapigano, Tahrir al-Sham, lililowekwa kwenye orodha ya makundi ya kigaidi ya Umoja wa Mataifa, liliwatimua mahasimu wao kwa zaidi ya kutoka thelathini ikiwa ni pamoja na mji wa Idleb. Mapigano haya yalisababiodsha vifo vya watu zaidi ya mia moja kutoka kambi zote mbili.

Wanajihadi wa kundi la Tahrir al-Cham wamechukua udhibiti wa utawala wote wa Idleb, ikiwa ni pamoja na vituo vya nishati, magereza na mahakama, baada ya kuwapokonya silaha walinzi.

Masaa kadhaa baada ya kuondoka kwa kundi la Ahrir al-Sham, mlipuko mkubwa ulisikika katika mji wa Idleb, wakati mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliingia katika kundi la wapiganaji wa Ahrir al Cham, ambao walikua wakibeba kiasi kikubwa cha silaha ma risasi. Shambulizi hilo lilisababisha vifo vya watu 11, kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu la OSDH, huku televisheni ya kiarabu ya al-Mayadeen ikiarifu watu 50 waliuawa katika shambulizi hilo.

kwenye ukurasa wake wa Twitter, Mohammad Allouch, ambaye anaongoza ujumbe wa waasi mjini Geneva, alionya wakazi wa Idleb dhidi ya udhibiti wa wanajihadi, hali ambayo inaweza kuubadilisha mji huo kama ule wa Mosul, ulioharibiwa katika mapigano.