Zaidi ya wapiganaji 11,000 kuondolewa kwenye mpaka wa Syria na Lebanon

Zaidi ya wapiganaji 1,000 kuondolewa kwenye mpaka wa Syria na Lebanon

Mabasi yanayotarajia kuwasafirisha wapiganaji wa kundi la zamani la al-Nosra Front yaliwasili kwenye mpaka kati ya Lebanon na Syria, Jumatatu, Julai 31.
Mabasi yanayotarajia kuwasafirisha wapiganaji wa kundi la zamani la al-Nosra Front yaliwasili kwenye mpaka kati ya Lebanon na Syria, Jumatatu, Julai 31. REUTERS/Ali Hashisho

Zaidi ya mabasi mia moja yaliwasili nchini Lebanon tangu siku ya Jumatatu kutoka nchini Syria. Mabasi hayo yameegesha katika mji wa Ersal kwenye mpaka wa Syria na Lebanon kwa monajili ya kuwaondoa wapiganaji na raia wa kawaida 11,000 kuanzia Jumanne hii Agosi mosi.

Matangazo ya kibiashara

Hili ni zoezi la kwanza la kuwaondoa wapiganaji na raia wa kawaida wa Syria waliopiga kambia katika nchi ya Lebanon tangu kuzuka kwa mapigano nchini Syria, mnamo mwaka 2011. Hizi ni mbili mbili tofauti.

Zoezi la kwanza linahusu wanajihadi 500 wa kundi la zamani la Al-Nosra Front, familia zao na raia wengine, ambao wameamua kwenda pamoja nao. Watu hao wanaokadiriwa kufikia 8000, watasafirishwa Jumanee hii kuelekea mkoa wa Idleb, kwa kutumia njia inayopita katika ardhi ya Syria. Msafara huo utashindikizwa na magari ya shirika la msalaba mwekundu kutoka Syria.

Watakapo wasili katika mji wa Aleppo, wanajihadi hao wa kundi la zamani la Al-Nosra Frontj watawaachia huru wapiganaji wanane wa Hezbollah. Watatu miongoni mwao walikamatwa wakati wa mapigano wiki iliyopita nchini Lebanon, na wengine 5 walikamatwa katika eneo la Aleppo, mwishoni mwa mwa mwaka 2016.

Operesheni nyingine inahusu wapiganaji 500 wa kundi la Saraya Ahl al-Sham, na watu 2 500 kutoka familia zao. Waliamua kurudi katika miji na vijiji vyao katika eneo la Qalamoun, nchini Syria, si mbali na mahali walipokuwa walikimbilia kwa miaka kadhaa.

Hezbollah na serikali ya Syria ndio walisaidia kuhitimisha makubaliano ya kurudi kwa kundi hili. Waasi hawa wataendelea kushikilia silaha zao ndogo ndogo baada kuahidi kusitisha mapigano dhidi ya jeshi la Syria.