SYRIA-IS-USALAMA

Jeshi la Syria kuangusha utawala wa IS

Gari la jeshi la Syria karibu na mji wa Deir Ezzor, tarehe 12 Novemba 2016.
Gari la jeshi la Syria karibu na mji wa Deir Ezzor, tarehe 12 Novemba 2016. Ayham al-Mohammad / AFP

Jeshi la Syria linasema linaelekea kuwashinda wapiganaji wa kundi la Islamic State katika ngome ya mji wa Deir Ezzor. Jeshi la Syria limefanikiwa kuyarejesha kwenye himaya yake maeneo kahaa yaliyokuwa yakishikiliwa na kundi la IS.

Matangazo ya kibiashara

Deir Ezzor imekuwa ngome ya Islamic State kwa muda mrefu na ikiwa jeshi la Syria litafanikiwa kuwaondoa wapiganaji hawa, basi yatakuwa ni mafanikio makubwa katika vita dhidi ya kundi hili nchini gumo.

Ripoti zinasema kuwa tayari Islamic State wameacha eneo kubw ala ngome yao yenye utajiri mkubwa wa mafuta, wakati huu makabiliano yakiendelea.

Mji wa Deir Ezzor ukapakana pia ni Iraq, nchi ambayo pia kumekuwa na makabiliano kama haya na tayari miji ya Mosul na Tal Afar, imekombolewa.

Vikosi vya Syria vinaonekana kufanikiwa kutokana na uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wanajeshi wa Urusi.