Pata taarifa kuu
PAKISTAN-UCHAGUZI

Mke wa Nawaz Sharif ashinda uchaguzi mdogo wa ubunge

Kulsoom Nawaz (kushoto) achukua nafasi ya mumewe Nawaz Sharif kuwa Waziri Mkuu. Lakini amelazwa hospitali kwa ugonjwa wa saratani, binti yake Maryam Nawaz (kulia) ndio ambaye alifanya kampeni ya uchaguzi.
Kulsoom Nawaz (kushoto) achukua nafasi ya mumewe Nawaz Sharif kuwa Waziri Mkuu. Lakini amelazwa hospitali kwa ugonjwa wa saratani, binti yake Maryam Nawaz (kulia) ndio ambaye alifanya kampeni ya uchaguzi. AFP PHOTO/Arif ALI
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Mke wa aliyekua Waziri Mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif, aliyetimuliwa mamlakani Julai 28 kufuatia kesi ya rushwa inayohusiana na Panama Papers iliyomkabili, ameshinda uchaguzi mdogo wa ubunge katika kuwania kiti cha ubunge kilichoachwa na mumewe.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu unampa nafasi kiongozi wa zamani kuendelea na ushawishi wake katika serikali, lakini pia unatoa nafasi kwa upinzani kwa uchaguzi ujao.

Matokeo ya uchaguzi huu mdogo wa wabunge umeshrehekewa na serikali na upinzani nchini Pakistan. Kwa upande wa familia ya Waziri Mkuu Nawaz Sharif, ni ushindi wa kwanza tangu alipotimuliwa mamlakani mwezi Julai iuliyopita kwa kesi ya rushwa.

Kulsoom Nawaz, mke wa Sharif aliyechaguliwa mbunge, hakushiriki kampeni za uchaguzi. Muda mfupi baada ya kuwasilisha barua yake ya kuwania kiti hicho kiliyoachwa na mumewe, madaktari waligundua kuwa ana kansa ya koo. Binti yake Maryam Nawaz ndio aliyeongoza kampeni. Kwa mujibu wa Maryam Nawaz, ushindi huu ni uthibitisho kwamba raia wa Pakistan hawakubaliani na uamuzi wa Mahakama Kuu ambayo imemtimua babake na kuiweka nchi ya Pakistan katika mgogoro mkubwa wa kisiasa.

Chama cha PTI, kinachoongozwa na nyota wa zamani wa kriketi Imran Khan, kimechukua nafasi ya pili na kuandikisha rekodi bora ya historia yake katika eneo la Lahore. Matokeo ambayo yanaonyesha mapambano makubwa kati ya vyama viwili wakati wa uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika katika majira ya baridi yajayo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.