Kiongozi wa kundi la IS ajieleza katika sauti iliyorekodiwa

Kiongozi wa kundi la IS Abu Bakr al-Baghdadi, aonekana hadharani kwa mara ya kwanza, Julai 5, 2014.
Kiongozi wa kundi la IS Abu Bakr al-Baghdadi, aonekana hadharani kwa mara ya kwanza, Julai 5, 2014. REUTERS/Social Media Website via Reuters TV

Kundi la kigaidi Islamic State limetoa mkanda wa sauti uliorekodiwa na kiongozi wao Abu Bakr al-Baghdadi na kuashiria kuwa kiongozi huyo bado yupo hai.

Matangazo ya kibiashara

Mkanda huo wa sauti uliowekwa kwenye mtandao mmoja unaosadikika kuwa na mafungamano na kundi la Islamic State, Abu Bakr al-Baghdadi anasikika akizungumzia maswala ya sasa, kiasi cha kuonyesha kwamba ni mkanda mpya uliorikodiwa hivi karibuni.

Abu Bakr al-Baghdadi hajasikika tangu Novemba mwaka jana na hata kuonekana hadharani, ambapo mara ya mwisho alionekana hadharani ilikuwa mwaka 2014 wakati alipohutubia katika Muskiti wa Al Nur katika Mjini wa Mosul ambapo alitangaza utawala wa kikhalifa.

Akizungumza kuonekana kwa kiongozi huyo, kiongozi wa vikosi vya Marekani vinavyopambana na Islamic State Ryan Dillon, amesema Marekani inaamini kiongozi huyo bado yupo hai tofauti na mataifa ya Urusi na Iran yanayodai kiongozi huyo alishauawa.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Dana White ameeleza kwamba Marekani inafuatilia taarifa hizo kwa karibu kabla ya kuchukua hatua zaidi.

Hata hivyo kusikika kwa kiongozi huyo kunakuja wakati huu kindi hilo linalojiita Islamic State likiendelea kupata pigo kubwa katika maeneo mbalimbali iliokuwa ikikalia.