SYRIA-IS-USALAMA

IS yatimuliwa katika mkoa wa Hama, Syria

Jiji la Syria la Kafr Nabudah, katika jimbo la Syria la Hama, tarehe 11 Oktoba 2015. Vikosi vya Serikali vinajaribu kuweka kwenye himaya yao mji huo.
Jiji la Syria la Kafr Nabudah, katika jimbo la Syria la Hama, tarehe 11 Oktoba 2015. Vikosi vya Serikali vinajaribu kuweka kwenye himaya yao mji huo. REUTERS/Ammar Abdullah

Jeshi la Syria na washirika wake walifanikiwa siku ya Jumatano Oktoba Oktoba 4kuwatimua wapiganaji wa kundi la Islamic State katika ngome zao za mwisho katika mkoa wa Hama.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imekuja baada ya mwezi mmoja wa mapigano mabaya, yalitosababisha vifo vya watu 600 kutoka katika kambi zote mbili, kwa mujibu wa shirika la Haki za Binadamu nchini Syria la OSDH.

Kundi la Islamic State lilikua likidhibiti tangu miaka mitatu iliyopita theluthi moja ya mkoa wa Hama, ambao ulikua ni njia muhimu unaotumiwa kwa kusambaza chakula na vifaa vya kijeshi vya jeshi la Syria kwenda Aleppo, kaskazini, Homs, katikati, na Damascus kuelekea kusini.

Askari wa Serikali walifaulu, katika hatua ya kwanza, kugawa mara mbili eneo lenye zaidi ya kilokilomita mraba 5,000 lililokua likidhibitiwa na wanamgambo wa Kiislamu kati ya mikoa ya Hama na Homs.

Mapema mwezi Septemba, jeshi la Syria lilizindua shambulio la mwisho dhidi ya mkoa wa Hama, kwa msaada wa kundi la Hezbollah kutoka Lebanon, watu waliojitolea kutoka Irani na vikosi maalum vya anga vya Urusi.

Mapigano hayo yameua watu zaidi ya 400 katika safu ya wapiganaji wa Kiislamu na 190 upande wa jeshi la Syria na washirika wake, amearifu mwandishi wetu huko Beirut, Paul Khalifeh.