YEMEN-USALAMA

Polisi zaidi ya 23 wauawa na IS nchini Yemen

Vikosi vya Yemen katika eneo la shambulio,  Aden, Novemba 5, 2017.
Vikosi vya Yemen katika eneo la shambulio, Aden, Novemba 5, 2017. STRINGER / AFP

Vikosi vya usalama vya Yemen vimedai kusitisha shambulio la Aden lililodaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State, na hivyo kuwadhibiti baadhi ya wapiganaji wa kundi hilo, licha ya polisi zaidi ya 23 kuuawa.

Matangazo ya kibiashara

Makao makuu ya kitengo cha polisi ya Jinai katika eneo la Aden, mjii mkubwa kusini mwa Yemen yalishambuliwa siku ya Jumapili na wapiganaji wa kundi la Islamic State ambao walifaulu kuingia katika jengo hilo, huku wakilichoma moto na kuchukua idadi isiyojulikana ya mateka , ikiwa ni pamoja na polisi wawili wa kike ambao walipigwa risasi.

Kwa jumla, polisi 23 waliuawa katika operesheni hiyo , amesema Jumatatu hii afisa wa usalama.

Vikosi vya usalama vilijaribu mara tatu wakati wa usiku kurejesha jengo hilo kwenye himaya yao, na kila wakati, mshambuliaji wa kujitoa mhanga alikua akijilipua na hivyo kuwazuia kuendelea, ameelezea afisaa huyo wa polisi.

Mshambuliaji wanne wa kujitoa mhanga alijilipua mapema Jumatatu asubuhi, lakini vikosi vya usalama vimefaulu kudhibiti hali ya mambo na kusitisha hali hiyo, kwa mujibu wa chanzo hicho.