SAUDI ARABIAUNSC-YEMEN-USALAMA-HAKI

Baraza la Usalama laagiza kuondolewa kwa vizuizi Yemen

Hali ya kibinadamu yaendelea kuzorota katika hospitali ya Sanaa, Yemen.
Hali ya kibinadamu yaendelea kuzorota katika hospitali ya Sanaa, Yemen. REUTERS/Mohamed al-Sayaghi

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeutaka muungano wa jeshi la nchi za Kiarabu linaloongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen kuondoa vizuizi katika maeneo muhimu na hivyo kuruhusu misaada ya kibinadamu kupelekwa tena nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa shirika la misaada la Umoja wa Mataifa Mark Lowcock ameonya kutokea kwa kubwa la njaa, iwapo misaada haitapelekwa Yemen.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeagiza kuondolewa kwa vizuizi hivyo kwa kusema kwamba hali ya kibinadamu ni ya kutisha.

Saudi Arabia na washirika wake wanaoendesha vita nchini Yemen wamefunga njia zote za ardhini, angani na za majini tangu siku ya Jumatatu. Saudi Arabia inabaini kwamba uamuzi huo ulichukuliwa kufuatia mashambulio ya makombora yaliyorushwa katika mji wa Riyadh na waasi wa Houthi kutoka Yemen.

Muungano wa nchi za Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia umetetea uamuzi wake ukisema kuwa vizuizi vinahitajika kuweza kuizuia Iran kuwapatia silaha waasi wa Ki-Houthi.

Mapema mwezi huu kombora la masafa marefu lilirushwa kwa kulenga uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mfalme Khalid, kwa mujibu wa televisheni ya wapiganaji wa Houthi ya Al-Masirah, lakini Saudi Arabia ilitungua kombora hilo, kwa mujibu wa duru kutoka jeshi la wanahewa la Saudia.