LEBANON-SAUDI ARABIA-USHIRIKIANO

Lebanon: Hariri anaonekana kuzuiliwa Saudi Arabia

Bango lililowekwa picha ya Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon, Saad Hariri, iliyowekwa kwene jengo lmoja mjini Tripoli, Libya.
Bango lililowekwa picha ya Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon, Saad Hariri, iliyowekwa kwene jengo lmoja mjini Tripoli, Libya. REUTERS/Omar Ibrahim

Serikali ya Lebanon inaona kuwa Saad Hariri ambaye alitangaza kwa mshangao mkubwa kujiuzulu kwenye nafasi ya waziri mkuu,yuko kizuizini nchini Saudi Arabia, chanzo rasmi cha serikali mjini Beirut kimesema.

Matangazo ya kibiashara

Katika muktadha huu, Lebanon itaanzisha mchakato katika baadhi ya nchi ili kushinikiza Saudi Arabia kumwachilia, chanzo hicho kimeongeza.

Saad Hariri alitangaza kujiuzulu siku ya Jumamosi iliyopita katika hotuba ya televisheni iliyorekodiwa mjini Riyadh, nchini saudi Arabia, akisema kuwa ana hofu ya kuuawa. alishtumu Iran na kundi la Hezbollah kuchochea migawanyiko katika ukanda huo.

Kujiuzulu kwake kulionekana kama hali ya mapambano ya miaka kadhaa kati ya utawaa wa kifalme wa Wahhabi na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, baina ya jamii ya Sunni na Shia nchini Iraq, Syria na Yemen.

Saudi Arabia kama jamaa ya Saad Hariri wamekanusha kuzuiliwa kwa aliyekua waziri mkuu wa Lebanon lakini Saad Hariri yeye mwenyewe hajatoa taarifa yoyote kuhusiana na madai hayo.