SAUDI ARABIA-LEBANON-USHIRIKIANO-USALAMA

Saudi Arabia yawataka raia wake kuondoka Lebanon

Mwanamfalme Mohammed bin Salman (kushoto) na Emmanuel Amcron walikutana Riyadh.
Mwanamfalme Mohammed bin Salman (kushoto) na Emmanuel Amcron walikutana Riyadh. AFP/Getty Images

Saudi Arabia imewataka raia wake waishio nchini Lebanon kuondoka mara moja nchini humo. Uamuzi huo uliochukuliwa siku ya Alhamisi iunakuja siku chache baada ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon, Saad Hariri kutangaza kujiuzulu. Uamuzi ambao ulipokelewa kwa mshangao mkubwa na serikali ya Lebanon.

Matangazo ya kibiashara

Chanzo cha Wizara ya Mambo ya Nje, kilichonukuliwa na shirika la habari la serijkali SPA, pia imewataka raia wa Saudi Arabia kutotembelea au kusafiri nchini Lebanon, akieleza kuwa "hali" nchini humo si shwari, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

Wakati huo huo Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye yuko nchini Saudi Arabia, amesema atasisitizia umuhimu wa utulivu nchini Lebanon, katika mazungumzo yake na na viongozi wa nchi hiyo.

Ufaransa ina uhusiano wa karibu na Lebanon, na ziara hiyo ya Rais Macron imekuja siku moja baada Saad Hariri, kujiuzulu wakati alipokuwa Riyadh, hali inayochochea hisia kwamba alishinikizwa na Saud Arabia.

Amesema pia atazungumza na viongozi wa Saudi Arabia kusaidia kuzuia baa la njaa nchini Yemen, ambako muungano wa majeshi yanayoongozwa na nchi hiyo yamefunga bandari kuzia silaha kuingizwa nchini humo na kuwafikia wapiganaji wa Ki Houthi.

Kwa kweli, wakati nchi inawataka wananchi wake kuondoka nchi ambako wanaishi, hii sio ishara nzuri. Kuna uwezekano wa kutokea vita kati ya nchi hizi mbili, wakati ambapo uhusiano si mzuri kati ya Lebanon na Saudi Arabia.

Lebanon imechukua miaka mingi ili kuwa na rais na waziri mkuu katika hali ya kushirikiana kuendelea taasisi zake. Mapema wiki hii waziri mkuu wa Lebanon alitangaza mjini Riyadh kuwamba anajiuzulu kwenye wadhifa wake na hivyo kuacha pengu kubwa katika nchi ambapo usawa wa jamii umekua ni tete.