LEBANON-SAUDI ARABIA-USHIRIKIANO

Saad Hariri: Niko huru Saudi Arabia

Waziri Mkuu wa Lebanon aliyejiuzulu Saad Hariri alizungumza kwa mara ya kwanza tangu alipojiuzulu mjini Riyadh wiki moja iliyopita.
Waziri Mkuu wa Lebanon aliyejiuzulu Saad Hariri alizungumza kwa mara ya kwanza tangu alipojiuzulu mjini Riyadh wiki moja iliyopita. FUTURE TV / AFP

Kwa mara ya kwanza tangu kujiuzulu kwake kutoka Riyadh mnamo Novemba 4, Waziri Mkuu wa Lebanon amefanya mahojiano kwenye kituo chake cha televisheni cha FTV. Bw. Hariri alitangaza kwamba atarejea nchini Lebanon "siku zijazo", bila kutoa tarehe maalum.

Matangazo ya kibiashara

Saad Hariri alisema yuko "huru" nchini Saudi Arabia, wakati ambapo serikali ya Beirut inaiomba Saudi Arabia kutoa maelezo kuhusu ya hali ya waziri mkuu aliyejiuzulu.

Saad Hariri alikubali tangazo lake la kujiuzulu akiwa nje ya nchi ni kuinyume na Katiba na hivyo kusema kuwa atawasilish abarua yake ya kujiuzulu kwa rais wa Lebanon. Hili ndilo ambalo nataka kufanya wakati nitarejea Beirut katika siku zijazo, amesema, bila kutoa tarehe maalum ya kurudi kwake.

Lengo la kujiuzulu kwake ilikuwa kutazama "maoni", kutoka wananchi wa Lebanon kuhusu hatari ambazo nchi hiyo inakabiliana nazo. Kwa mujibu wa Hariri, hatari hizi zinatokana na kuingiliwa kwa masuala ya nchi za Kiaraba na kundi la Hezbollah, hasa vita vya Yemeni. Kutokua na upendeleo ni uwezekano wa kuhifadhi utulivu wa nchi, amesem aSaad Hariri.

Saad Hariri ameelezea ukimya wake kwa muda wa wiki akibaini kwamba alikua "akitafakari" baada ya uamuzi wake wa kujiuzulu. Akihojiwa kama yuko huru nchini Saudi Arabia Saad Hariri alihakikisha kwamba angeweza kurudi usiku wa jana kama angependa.