YEMEN-USALAMA

Shambulio la kujitoa mhanga laua watu zaidi ya sita Aden, Yemen

Yemen inaendelea kukabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya vikosi vya Kishia vya Houthi na serikali ya Rais wa Abd-Rabbou Mansour Hadi.
Yemen inaendelea kukabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya vikosi vya Kishia vya Houthi na serikali ya Rais wa Abd-Rabbou Mansour Hadi. STRINGER / AFP

Shambulio la kujitoa mhanga limegharimu maisha ya watu zaidi ya sita na kuwajruhi wengine wengi katika mji wa Aden, kusini mwa Yemen, mashahidi wamesema, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Matangazo ya kibiashara

Watu wawili waliokua ndani ya gari lililotegwa bomu walilipua gari lao karibu na kambi inayotumiwa na kikosi maalumu cha usalama cha Yemen, Security Belt, kilichoundwa na muungano wa nchi za Kirabu unaoongozwa na Saudi Arabia kwa vita dhidi ya waasi wa Houthi.

"Security Belt " iliundwa na Falme za Kiarabu (UAE) kusaidia kurejesha usalama katika mji wa Aden.

Watu wengi, ikiwa ni pamoja na raia wa kawaida, wamejeruhiwa.

Mashahidi wamesema kuwa mlipuko huo ulikua wenyenguvu kiasi kwamba ulitikisa eneo lote la Al Mansoura, kaskazini mwa Aden. Shambulio hilo limeharibu baadhi ya majengo.

Picha zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha vijana kadhaa wakivalia sare za kijeshi wakibebwa hospitalini katika magari ya wagonjwa.

Yemen inaendelea kukabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya vikosi vya Kishia vya Houthi vinavyosaidiwa na Iran na serikali ya Rais wa Abd-Rabbou Mansour Hadi anayetambuliwa na jumuiya ya kimataifa na kuungwa mkono na muungano wa Kiarabu unaoongozwa na Saudi Arabia.