LEBANON-SAUDI ARABIA-USHIRIKIANO

Saad Hariri kurejea Lebanon katika siku mbili zijazo

Mfalme Salman wa Arabia Saudi na Waziri Mkuu wa Lebanon aliejiuzulu Saad Hariri Jumatatu, Novemba 6, 2017,  Riyadh.
Mfalme Salman wa Arabia Saudi na Waziri Mkuu wa Lebanon aliejiuzulu Saad Hariri Jumatatu, Novemba 6, 2017, Riyadh. Saudi Press Agency/Handout via REUTERS

Waziri mkuu wa Lebanon Saad Hariri amefahamisha kuwa  atarejea nchini katika siku mbili zijazo ili kumaliza  masharti ya kujiuzulu. 

Matangazo ya kibiashara

Saad Hariri waziri mkuu wa Lebanon alietangaza kujiuzulu ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter kuwa atajielekeza nchini humo katika siku mbili zijazo kutokea nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kutimiza masharti kuhusu kujşuzulu kwake katika wadhifa wake.

Ili kuheshimisha katiba ya nchi Saad Hariri amesema kuwa ni wajibu kwake kujielekeza nchini Lebanon kujiuzulu rasmi.

Novemba 4 Saad Hariri alitangaza kujiuzulu katika wadhifa wake akiwa katika ziara nchini Saudi Arabia.

Washirika wake wanasema kuwa anashikwa mateka lakini Bw. Hariri anakana hayo.

Amelilaumu kundi linaloungwa mkono na Iran la Hezbollah kuwa sababu ya kujiuzulu kwake akisema alihofia usalama wake na wa familia yake.

Hariri ambaye na kiongozi wa Sunni na mfanyabiashara, aliteuliwa kuunda serikali ya Lebanon mwezi Novemba mwaka 2016.

"Nimejiuzulu. Ninaenda Lebanon hivi karibuni na nitajiuzulu kuambatana na Katiba ya nchi ya Lebanon," alisema wakati wa mahojiano ya televisheni,.

Kupitia hotuba iliyopeperushwa kwa njia ya televisheni kutoka mji wa Riyadh Bw. Hariri aliilaumu Iran na Hezbollah kwa kudhibiti Lebanon na kulivurujga eneo lote hilo.