AFGHANISTAN-IS-USALAMA

Shambulizi la kujitoa mhanga laua watu 9 Kabul, Afghanistan

Vikosi vya usalama vya Afghanistan kwenye eneo la tukio, Kabul.
Vikosi vya usalama vya Afghanistan kwenye eneo la tukio, Kabul. REUTERS/Mohammad Ismail

Watu wasiopungua tisa wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulizi la kujitoa mhanga mjini Kabul Alhamisi hii Novemba 16. Shambulizi hilo lililenga mkutano wa wafuasi wa kiongozi mmoja wa kisiasa, Wizara ya Mambo ya Ndani imebaini.

Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hili limedaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State (IS), kupitia shirika lake la propaganda, Amaq.

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alikaribia hoteli ambako kulikua kukifanyika mkutano wa wafuasi wa Atta Mohammad Noor katika eneo la Khair Khana na kujilipua. Polisi watani na raia wawili ni miongoni mwa watu waliouawa na shambulio hilo, Wizara hiyo imesema.

Noor ni gavana wa jimbo la Balkh, kaskazini mwa Afghanistan, na mmoja wa viongozi wa chama cha Jamiat-i-Islami, chenye watu wengi kutoka kabila ya Tajiki. Haijulikani ikiwa alikuwa katika eneo hilo wakati wa mlipuko.

Mvutano wa kisiasa unazidi kuongezeka nchini Afghanistan kuelekea uchaguzi wa urais wa mwaka 2019.

Siku ya Jumatano Rais Ashraf Ghani alimfuta kazi Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, hali ambayo inaweka mashakani kufanyika kwa uchaguzi wa wa wabunge mwaka ujao.