LEBANON-UFARANSA-SAUDI ARABIA-USHIRIKIANO

Saad Hariri atarajiwa kwenda Paris Jumamosi hii

Mfalme Salman wa Saudi Arabia na Waziri Mkuu wa Lebanoni aliyejiuzulu Saad Hariri Jumatatu, Novemba 6, 2017, Riyadh.
Mfalme Salman wa Saudi Arabia na Waziri Mkuu wa Lebanoni aliyejiuzulu Saad Hariri Jumatatu, Novemba 6, 2017, Riyadh. Saudi Press Agency/Handout via REUTERS

Waziri Mkuu wa Lebanon, Saad Hariri, ambaye yuko nchini Saudi Arabia tangu alipotangaza kujiuzulu kwake, anatarajiwa kusafiri kwenda ncini Ufaransa siku ya Jumamosi ambapo atakutana na Rais Emmanuel Macron.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili lililotolewa siku ya Alhamisi na ikulu ya Elysee Palace linakwenda sambamba na ziara ya Waziri wa mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian mjini Riyadh. Katika ziara hiyo Bw. Le Drian alikuatana na Saad Hariri, mwenye umri wa miaka 47. Aliingilia kati baada ya kukanushwa kwa Saudi Arabia kuhusu madai ya kuzuliwa kusafiri kwa Bw. Hariri.

Saad Hariri alitangaza kujiuzulu tarehe 4 Novemba akiwa mjini Riyadh akishtumu Iran nakundi la Hezbollah la Lebanon kuzorotesha usalama nchini Lebanon, na kuhofia kuongezeka kwa mvutano kati ya Saudi Arabia na Iran, nchi mbili zenye nguvu katika kanda ya Mashariki ya Kati kikanda.

"Elysee inathibitisha kuwasili nchini Ufaransa kwa Saad Hariri na mkutano na Rais Emmanuel Macron siku ya Jumamosi katika ikulu ya Elysee", Ofisi ya rais imeliambia shirika la habari la AFP.

Ufaransa, ambayo kihistoria ina uhusiano wa karibuna Lebanoni, hivi karibuni ilianzisha juhudi za kujaribu kutafuta njia ya kuondokana na mgogoro huo unaoikabili Lebanon.