IRAN-SYRIA-IS-USALAMA

Rais wa Iran atangaza kuvunjwa kwa kundi la IS

RAis wa Iran Hassan Rohani amesem akundi la IS limetokomezwa na halina nafasi tena.
RAis wa Iran Hassan Rohani amesem akundi la IS limetokomezwa na halina nafasi tena. REUTERS/Stephanie Keith

Rais wa Iran Hassan Rohani ametangaza leo Jumanne kwamba kundi la Islamic State limevunjwa. Kauli hiyo ameitoa katika hotuba yake iliyorushwa moja kwa moja kwenye televisheni ya serikali.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo la kuvunjwa kwa kundi la Islamic State limetolewa pia na Jenerali Qassem Soleimani, kiongozi mwandamizi wa vikosi vya jeshi la ulinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (GRI, pasdarans) katika ujumbe uliotumwa kwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislam, Ayatollah Ali Khamenei, ujumbe ambao ulirushwa kwenye tovuti ya vikosi hivyo, Sepah News.

Jeshi la Syria na washirika wake wamepata udhibiti kamili wa mji wa Albou Kamal, ngome ya mwisho ya kundi la Islamic State (IS) nchini Syria, idara ya mawasiliano ya Hezbollah kutoka Lebanon ilisema siku ya Jumapili.

Baada ya kushindwa katika mji wa Albu Kamal, kundi la Islamic State linashikilia tu vijiji kadhaa nchini Syria, pamoja na maeneo mengine yasiyokua muhimu nchini humo.