LEBANON-HEZBOLLAH-USALAMA

Saad Hariri asitisha uamuzi wake wa kujiuzulu

Saad Hariri, Waziri Mkuu wa Lebanon.
Saad Hariri, Waziri Mkuu wa Lebanon. AFP/Joseph Eid

Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri amesema hivi leo kuwa amesitisha uamuzi wake wa kujiuzulu aliotangaza mjini Riyadh, nchini Saud Arabia, mapema mwezi Novemba, kwa kusubiri mashauriano kuhusu masuala nyeti, ikiwa ni pamoja na Hezbollah kuingilia migogoro katika kanda ya Mashariki ya Kati.

Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu unatazamia kupunguza hali ya sintofahamu iliokua ikiendelea nchini humobaada yaSaad Hariri kutangaza kujiuzulu Novemba 4 mjini Ryad, ambako kusalia kwake kwa muda mrefu mjini humo kuliibua maswali mengi, huku viongozi wa Lebanon wakishtumu Saudi Arabia kumzuia ili asiwezi kurejea nchini.

Kauli hiyo ya kufuta uamuzi wake wa kujiuzulu Bw. Hariri aliitoa baada ya kukutana kwa mazungumzo na rais wa Lebanon Michel Aoun. Bw. Hariri amettaka kuepo na "majadiliano" kati ya vyama vya siasa nchini Lebanon, ambapo pande mbili zinahasimiana.

"Nilijadili kuhusu kujiuzulu kwangu na rais wa Jamhuri, lakini aliniomba nisubiri kabla ya kuwasilisha barua ya kujiuzulu ili kuruhusu mashauriano zaidi (...) Nimekubali ombi hilo", Bw Hariri amesema.

Mtaalam wa masuala ya katiba Edmond Rizk ameliambia shirika la habari la AFP kwamba "kama rais hajakubali uamuzi wa kujiuzulu, uamuzi wa Bw. Hariri utakua sio sahihi kisheria".