SYRIA-MAZUNGUMZO-SIASA

Ujumbe wa Damascus unatarajiwa katika mazungumzo ya Geneva

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Staffan de Mistura (wa 3 kutoka kushoto) akismsabahi kiongozi wa ujumbe wa kundi la upinzani Nasser al-Hariri wakati wa ufunguzi wa mazungumzo ya amani kuhusu Syria Geneva Novemba 28, 2017.
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Staffan de Mistura (wa 3 kutoka kushoto) akismsabahi kiongozi wa ujumbe wa kundi la upinzani Nasser al-Hariri wakati wa ufunguzi wa mazungumzo ya amani kuhusu Syria Geneva Novemba 28, 2017. REUTERS/Fabrice Coffrini/Pool

Ujumbe wa serikali ya Damascuas unatarajiwa leo Jumatano katika mazungumzo ya Geneva kuhusu Syria chini ya mwavuli wa Umoja wa Mataifa, siku moja baada ya mazungumzo hayo kuanza.

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa ulianza mazungumzo yake na upinzani wa Syria siku ya Jumanne. Lakini taarifa za upinzani zinazokudai rais Bashar al-Assad ajiuzulu zimekua zimesababisha serikali ya Syria kutuma ujumbe wake katika mazungumzo hayo. Serikali ya Syria kwa msaada wa Urusi imefanikiwa kushinda vita katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu na waasi.

Urusi, mshirika wa kijeshi na kisiasa wa serikali ya Syria, imeweza kushawishi utawala wa Bashar al-Assad kutuma ujumbe wake Geneva. Mwakilishi wa Urusi alitangaza mapema asubuhi, katika mkutano na wajumbe watano wa kudumu wa Baraza la Usalama, kusitisha kwa mapigano na jeshi la Syria katika eneo la Ghouta ya Mashariki , mkoa unaodhibitiwa na waasi karibu na Damascus.

Pamoja na ukosefu wa ujumbe wa Syria, Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Staffan de Mistura, ambaye tayari ameendesha bila mafanikio vikao saba vya mazungumzo mjini Geneva tangu 2016, alifungu siku ya Jumanne jioni kikao cha nane cha mazungumzo na ujumbe wa upinzani.

De Mistura amepanga leo Jumatano kukutana na balozi wa Syria kwenye Umoja wa Mataifa, Bashar al-Jaafari, mkuu wa ujumbe wa serikali ya Damascus.

Lakini kwa mujibu wa afisa mkuu wa Syria, mazungumzo yao yatakua hasa ni fursa kwa serikali ya Damascus ya kukataa kujadili hatima ya rais Assad.

Balozi wa Syria kwenye Umoja wa Mataifa (UN) na Mkuu wa ujumbe wa Serikali ya Syria Bashar al-Jaafari (kushoto) na Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Staffan de Mistura (kulia) Geneva, Machi 16, 2016.
Balozi wa Syria kwenye Umoja wa Mataifa (UN) na Mkuu wa ujumbe wa Serikali ya Syria Bashar al-Jaafari (kushoto) na Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Staffan de Mistura (kulia) Geneva, Machi 16, 2016. REUTERS/Philippe Desmazes/Pool