LEBANON-HEZBOLLAH-SIASA-USALAMA

Saad Hariri kuendelea kushikilia wadhifa wake wa waziri mkuu

Saad Hariri amerejelea kauli yake ya kuendelea kushikilia nafasi yake ya waziri mkuu wa Lebanon.
Saad Hariri amerejelea kauli yake ya kuendelea kushikilia nafasi yake ya waziri mkuu wa Lebanon. /REUTERS/Egyptian Presidency

Saad Hariri aliyetangaza kujiuzulu kwenye nafasi yake wa waziri mkuu wa Lebanon akiwa ziarani nchini Saudi Arabia amehakikisha kuwa ataendelea na wadhifa huo.

Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano yaliyochapishwa leo Alhamisi katika gazeti la Paris Match, Bw Hariri amesema alijiuzulu ili "ulimwengu uelew kuwa Lebanon haiwezi kuvumilia " Hezbollah kuingilia kati katika masuala ya nchi mbalimbali za ukanda wa Mashariki ya Kati.

Saad Hariri, ambaye alitangaza kujiuzulu tarehe 4 Novemba akiwa nchini Saudi Arabia akishtumu uharibifu unaofanywa na Iran na Hezbollan kutoka Lebanon, alikubali "kurejelea" uamuzi wake baada ya kurejea katika mji wa Beirut Novemba 21.

Alipoulizwa katika gazeti la Paris Match kama ataendelea kushikilia nafasi yake ya waziri mkuu, Saad Hariri alijibu "ndiyo".

"Nilijiuzulu nikiwa Riyadh kwa nia ya kuona jinsi gani uamuzi wangu utapokelewa nchiniLebanon," Bw Hariri amesema.

"Nilitaka ulimwengu kuelewa kwamba Lebanon haiwezi kuvumilia chama kama Hezbollah kuingilia katika masuala ya nchi za Ghuba, ambapo wanaishi watu 300,000 wa Lebanon," Saad Hariri ameongeza. "Hatupaswi kuangaliwa kwa vibaya kutokana na vitendo vya Hezbollah."

"Sintokukubali chama chochote cha siasa cha Lebanon kushiriki katika harakati zozote kwa maslahi ya Iran," Bw. Hariri amesema.