SYRIA-UN-USALAMA

Umoja wa Mataifa watoa wito kwa Wasyria kupiga hatua katika mazungumzo yao

Msuluhishi wa mazungumzo kati ya Wasyria kutoka Umoja wa Mataifa Staffan De Mistura.
Msuluhishi wa mazungumzo kati ya Wasyria kutoka Umoja wa Mataifa Staffan De Mistura. REUTERS/Pierre Albouy

Mazungumzo magumu kutatua mzozo wa miaka sita nchini Syria yanatarajiwa kuanza rasmi baada ya ujumbe wa serikali ya Syria kuwasili jijini Geneva.

Matangazo ya kibiashara

Msuluhishi wa mazungumzo hayo kutoka Umoja wa Mataifa Staffan De Mistura, ametaka pande zote mbili kudhamiria kupiga hatua.

Serikali ya Syria ilikubali kushiriki katika mazungumzo hayo kwa masharti kuwa, suala la rais Bashar Al Assad kuondoka madarakani halijadiliwi. Hata hivyo upinzani unamtaka Assad kuondoka.

Mapema wiki hii Mratibu wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, Staffan de Mistura, alitangaza kwamba alikuwa amejulishwa siku ya Jumapili jioni kuahirishwa kwa ujio wa ujumbe rasmi wa serikali ya Syria katika mazungumzo ya Geneva.

Pamoja na hali hiyo, Staffan de Mistura, ambaye tayari amefanya vikao 7 vya mazungumzo kati ya Wasyria mjini Geneva tangu mwaka 2016, bila mafanikio, bado ana matumani ya kupatikana kwa suluhisho katika mgogoro wa Syria. Anatarajia kuondoa hali inayotanda katika mchakato wa Geneva, kwa mara ya kwanza, kutokana na kushiriki kwa mara ya kwanza ujumbe mmoja wa upinzani wa Syria, unaowakilisha makundi yake yote, ikiwa ni pamoja na makundi yenye msimamo wa wastani, ambayo serikali ya Damascus inaona kuwa si tishio kwake.

Mnamo mwezi Septemba, De Mistura aliutaka upinzani wa Syria kuwa waangalifu kwa madai yao kwa sababu hawakushinda vita." Ikimaanisha kutodai tena kwamba suluhisho la mgogoro wa Syria ni kujiuzulu kwa rais Bashar Al Assad.