SYRIA-MAZUNGUMZO-SIASA

Umoja wa Mataifa wailamu Syria kusababisha kuvunjika kwa mazungumzo

Msuluhishi wa mzozo wa Syria Staffan de Mistura Staffan de Mistura.
Msuluhishi wa mzozo wa Syria Staffan de Mistura Staffan de Mistura. REUTERS/Pierre Albouy

Msuluhishi wa mzozo wa Syria Staffan de Mistura amesema mazungumzo ya amani kati ya wapinzani na serikali ya Syria yaliyokuwa yanaendelea jijini Geneva yamevunjika.

Matangazo ya kibiashara

Mistura ameilaumu serikali ya Syria kwa kusababisha kuvunjika kwa mazungumzo haya, na kusema ni kukosa nafasi ya thamani.

Msuluhishi huyo ameeleza pia kwamba upande wa serikali ulikataa, kujadili suala lingine kando na namna ya kupambana na ugaidi nchini humo.

Tangu mzozo wa Syria karibu miaka sita iliyopita, mazungumzo yamefanyika mara saba na kwa nyakati hizo zote, hakuna mwafaka wowote uliopatikana.

Upande wa upinzani na serikali haujawahi kukutana ana kwa ana huku kila upande ukishikilia msimamo wake.

Upinzani unataka rais Bashar Al Assad kuondoka madarakani, huku serikali ya Damascus ikisema kiongozi huyo hawezi kuondoka.

Maelfu ya wananchi wa Syria wamepoteza maisha na mamilioni kusalia wakimbizi katika mgogoro huo.