ISRAEL-GUATEMALA-PALESTINA-USHIRIKIANO

Benjamin Netanyahu akaribisha hatua ya Jimmy Morales juu ya Jerusalem

Waziri Mkuuwa Israel Benjamin Netanyahu ampongeza rais wa Guatemala Jimmy Morales kwa hatua ya kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.
Waziri Mkuuwa Israel Benjamin Netanyahu ampongeza rais wa Guatemala Jimmy Morales kwa hatua ya kutambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel. REUTERS/Amir Cohen

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekaribisha uamuzi wa rais wa Guatemala Jimmy Morales wa kuhamisha ubalozi wa nchi yake nchini Israeli Katika mji wa Jerusalem.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili rais wa Guatemala alitangaza kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa anatarajia kuhamisha ubalozi wa nbchi yake nchini Israel katika mji wa Jerusalem, baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Israel. Jimmy Morales anakuwa rais wa kwanza kuchukuwa uamuzi sambamba na ule uliotangazwa na Donald Trump mapema mwezi Desemba.

"Mungu akubariki, rafiki yangu, rais Jimmy Morales. Milikuambia hivi hivi karibuni kwamba nchi nyingine zitatambua Jerusalemu kama mji mkuu wa Israel na kutangaza kuhamisha ofisi zao ubalozi katika mji huo. Guatemala ni nchi ya pili kuchukua uamuzi huo, huo ni mwanzo kuna nchi nyingi tu zitafanya hivyo, "amesema Benjamin Netanyahu.

Siku ya Ijumaa, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ulipiga kura kushtumu mpango wa Marekani wa kuhamisha ubalozi wake katika mji wa Jerusalem. Nchi tisa ikiwa ni pamoja na Israeli, Marekani na Guatemala zilipinga azimio hilo. Palestina imesema uamuzi wa Guatemala ni kitendo cha aibu.

"Uamuzi huo ni sehemu ya ukiukwaji wa sheria ya kimataifa ambayo inakataza kuambatanisha maeneo yanayo kaliwa na Wayahudi. Uamuzi huu haubadili chochote. Ukweli ni kwamba nchi nyingi duniani zinapinga kuhamisha ofisi zao za ubalozi na zinapinga kutambua Jerusalem mashariki kama mji mkuu wa Israel. Nchi nyingi ziko upande wetu na uamuzi wa nchi kama Guatemala hautababadili chochote, "amesema Mustafa Barghouti.

Uamuzi wa Donald Trump wa Desemba 6 ulisababisha maandamano makubwa yanayofanyika kila siku katika maeneo ya Palestina. Msimamo wa Umoja wa Mataifa haujabadilika. Umoja huo hautambui mji wa Jerusalem mashariki kama sehemu ya Israel.

Wakati huo huo Israel inashauriana na mataifa 10, ili yahamishe balozi zao kutoka mjini Tel Aviv hadi Jerusalem.

Naibu Waziri wa Mambo ya nje wa Isarel Tzipi Hotovely amesema kuwa miongoni mwa mataufa hayo ni kutoka barani Ulaya.

Yote haya yanakuja baada ya Marekani, kutangaza hivi karibuni kutambua Jerusalem kuwa makao makuu ya Israel, hatua ambayo imeikasirisha Palestina na mataifa mengine ya Kiarabu.